canti in swahili

Baba Yetu (jina lako)
(lingua: Swahili – Kenya)

Jina lako, Baba, litukuzwe,
utawale petu milele yote
Baba yetu mwema uliye mbinguni
Jina lako, Baba, litukuzwe,
Na ufalme wako uje mapo kwetu,
na mapenzi yako yatimilike
Tupe leo mkate wa kila siku,
tupe leo mkate wa kila siku
Na utusamehe makosa yetu,
kama tufanyavyo kwa ndugu zetu
Situtie, Baba, kishawishini,
bali maovuni utuopoe
Ufalme na nguvu nao utukufu,
vyote vyako, Baba, hata milele

Il Tuo nome, Padre, sia santificato
Padre nostro buono che sei nei cieli
Sia santificato il Tuo nome,
venga il Tuo regno tra noi
sia fatta la Tua volontà
Dacci oggi il pane di ogni giorno
Perdona i nostri peccati
così come li perdoniamo ai nostri fratelli
Non ci indurre in tentazione ma liberaci,
dal male liberaci,
Perché venga il Tuo grande Regno
Ora e sempre, Padre, e così sia

 

 

Baba Yetu (uliye mbinguni)
(lingua: Swahili – Kenya)

(Baba yetu)
Baba, uliye mbinguni (2v)
Jina lako litukuzwe, ufalme wako ufike,
utakalo lifanyike, duniani kama mbinguni
Tupe leo riziki zetu, riziki za kila siku,
tusamehe makosa yetu,
kama tunavyowasamehe nasi waliotukosea.
Situtie majaribuni, walakini utuopoe,
tuopoe maovuni, tuopoe maovuni.
Kwa kuwa ‘falme, ufalme ni Wako,
na nguvu, utukufu milele,
utukufu milele, utukufu milele.

Padre nostro che sei nei cieli
Sia santificato il tuo nome,
venga il tuo regno
sia fatta la tua volontà
in cielo come in terra
Dacci oggi il nostro riso, il riso di ogni giorno
Perdona le nostre mancanze
così come noi le perdoniamo a chi le commette
Non ci indurre in tentazione ma liberaci,
dal male liberaci, liberaci!
Perché venga il Tuo regno, il regno è Tuo
E forte e grandioso sia, che sia grandioso!

 

 

Ee Bwana Tunakutolea
(lingua: Swahili – Tanzania)
Ee Bwana tunakutolea
Ee Bwana tunakutolea sadaka yetu
uibarikie Bwana na ipokee
Humu umo mkate wetu ee Bwana tunakutolea
Uukubali, uubariki uupokee
Tuna ubani yetu ee Bwana tunakutolea
Uikubali, uibariki uipokee
Humu zimo sala zetu ee Bwana tunakutolea
Uzikubali, uzibariki na uzipokee

O Signore ti offriamo
O Signore ti offriamo le nostre offerte
Accettale, benedicile e ricevile, Signore
Insieme al nostro pane, accettaci Signore
Insieme al nostro incenso, accettaci Signore
Insieme alle nostre preghiere, accettaci Signore

 

 

Fumbo La Imani
(lingua: Swahili – Tanzania)

Fumbo la imani, twalitangaza
duniani popote e popote e popote
Alivyo ufia ulimwengu
alivyo ukomboa, kwa damu, kwa damu
(kweli Bwana) kuzimuni, (Bwana), alishuka (kweli Bwana)
na mauti (Bwana), kayashinda
(kweli Bwana)
kweli Bwana, alifuka, alifuka, alifuka
Bwana alifufuka, (a), fufuka, (a), fufuka
Bwana atarudia, (a), rudia, (a), rudi

Mistero della Fede, lo proclamiamo
In tutti gli angoli del mondo
è morto per il mondo
così ci ha salvato con il suo sangue

 

 

Ingia
(lingua: Swahili – Kenya)

Ingia, ingia, ingia, ingia,
Ingia, ingia, uwe mmoja wa kondoo
Padre ingia, sista ingia,
shemasi ingia uwe mmoja wa kondoo
Baba ingia, mama ingia,
vijana waingie uwe mmoja wa kondoo
Ndege waingie, wanyama ingia,
wote waingie uwe mmoja wa kondoo

Entrate, entrate!
Siate i primi tra le pecorelle
entra missionario, entra missionaria, entra maestro,
siate i primi tra le pecorelle
entra Padre, entra madre,
entrate giovani siate i primi tra le pecorelle
entrate colombe, entrino i buoi,
che entrino tutti per stare tra le pecorelle

 

 

Kyrie-e
(lingua: Swahili – Tanzania)

E -e Bwana, e Bwana utuhurumie sisi
tuwakosefu utuhurumie
E -e Kristu, e Kristu utuhurumie sisi
tuwakosefu utuhurumie

Oh Signore
Oh Signore perdonaci
perchè abbiamo peccato perdonaci
Oh Cristo
Oh Cristo perdonaci
perchè abbiamo peccato perdonaci

 

 

Mtakatifu
(lingua: Swahili – Tanzania)

Mtakatifu Bwana Mungu wetu
mtakatifu Bwana wa majeshi
Mbingu na dunia zimejaa
utukufu wako ee Bwana
Hosana, hosana, hosana hosana (2v)
Mbarikwa yeye mwenyekuja
kwa jina la Bwana, hosana

Santo è il Signore nostro Dio
Santo è il Signore degli eserciti
il cielo e la terra sono pieni
della Tua gloria o Signore
Benedetto colui che viene
nel nome del Signore

 

 

Mwokozi Bwana Amefufuka
(lingua: Swahili – Tanzania)

Njooni wapenzi tufanye shangwe
mwokozi Bwana amefufuka
viumbe vyote vifanye shangwe
mwokozi Bwana amefufuka
Na tufanye shangwe, twimbe aleluya
mwokozi Bwana amefufuka (2v)
Hakika mbingu zishangilia mwokozi Bwana amefufuka
nayo dunia yafanya shangwe mwokozi Bwana amefufuka
Juu mbinguni na duniani mwokozi Bwana amefufuka
Viumbe viote vinafurahi mwokozi Bwana amefufuka
Hii ni siku aliyofanya mwokozi Bwana amefufuka
Tunafurahie tushangilie mwokozi Bwana amefufuka

Il Signore Salvatore è risorto
venite tutti carissimi, facciamo festa
il Signore è risorto
tutte le creature facciamo festa
Facciamo festa, cantiamo alleluia
il Signore è risorto
Veramente in cielo si gioisce
pure la terra fa festa
In cielo e in terra
tutte le cose gioiscono
Questo è il giorno fatto da Lui
godiamo ed esultiamo
Facciamo festa con dei canti
lodiamo il Signore e adoriamolo
Perchè è grande e santo
è Re, Signore di tutte le cose

 

 

Mungu Ibariki
(lingua: Swahili – Tanzania)

Mungu ibariki Afrika
wabariki viongozi wake
hekima na umoja na amani
Mungu ibariki Afrika na watu wake
Ibariki Afrika , Ibariki Afrika
Wabariki watoto wa Afrika
Mungu ibariki Afrika
dumisha uhuru na umoja
wake kwa waume na watoto
Mungu ibariki Afrika na watu wake
Ibariki Afrika, Ibariki Afrika
Tunabariki watoto wa Afrika

Il Signore Dio benedica l’Afrika
Benedica i suoi governanti
con la sapienza, l’unità e la pace
Dio benedica L’Afrika e la sua gente
sia benedetta L’Afrika
siano benedetti i bambini dell’Afrika

 

 

Napenda sana
(lingua: Swahili – Congo RD)

Napenda sana!
Napenda yo, yo, yo, yo – napenda
Jeruzalemu mji wa Baba Mungu, napenda
Neno lako, ee Baba
Nasikia mimi moyoni mwangu, ee Baba
Sauti yako, ee Baba
Yanipendeza sana na cheka mimi, e Baba
Mapendo yako, ee Baba
Yanapita ubaya wetu sisi, ee Baba

Ti voglio tanto bene
Ti voglio bene, yo, yo, yo, yo, ti voglio bene
grande città di Dio Padre,
Gerusalemme, ti voglio bene
La Tua parola, o Padre
la ascolto nel mio cuore, o Padre
La Tua voce, o Padre
Mi fa molto piacere e ne gioisco
Il Tuo amore, o Padre
supera la nostra cattiveria, o Padre

 

 

Neno Litasimama
(lingua: Swahili – Kenya)

Neno litasimama
neno litasimama
ya ulimwengu yatapita
lakini neno litasimama (neno)
Uovu wote utapita
umaskini utapita
ya ulimwengu yatapita
lakini neno lake bwana litasimama (neno)
Lujana wako utapita
uzee wako utapita
ya ulimwengu yatapita
lakini neno lake bwana litasimama (neno)
Maisha yote yatapita
na kila mtu atafuka
ya ulimwengu yatapita
lakini neno lake bwana litasimama (neno)

La parola di Dio non passerà
passerà questo mondo e tutto il male
Passerà la cattiveria e la povertà
Passeranno i nostri tempi
Passeranno la vita e la morte

 

 

Nifanye Hima Bwana
(lingua: Swahili – Kenya)

Nifanye hima Bwana
Nifanye hima Bwana
Niende nikakusifu kwa maana unanipenda
Ukura nimekataa (kabisa)
ulevi nimekataa
katika jina la Yesu
kwa maana unanipenda
Rama nimekataa (kabisa)
amaza nimekataa
katika jina la Yesu kwa maana unanipenda
Banki nimekataa (kabisa)
siasa nimekataa
katika jina la Yesu kwa maana unanipenda

Il Signore può tutto
ed io voglio lodarlo
perchè Lui mi ama
Nulla può farmi male
(assolutamente)
nel nome di Gesù
perchè Lui mi ama

 

Nitasimama
(lingua: Swahili – Tanzania)

Nitasimama nitasimama, Bwana e-e-ee
nitasimama kwa wito wako
Nilikuwa mbele mkosefu sana
nikatembelea kwa njia ya Bwana
unisimamishe ee Bwana
Nilikuwa mbele mlevi sana
nikatembelea kwa njia ya Bwana
unisimamishe ee Bwana
Nilikuwa mbele mpubavu sana
nikatembelea kwa njia ya Bwana
unisimamishe ee Bwana
Nilikuwa mbele mzaifu sana
nikatembelea kwa njia ya Bwana
unisimamishe ee Bwana
Nilikuwa mbele mdhaifu sana
nikatembelea kwa njia ya Bwana
umisimamishe ee Bwana.

Mi alzerò davanti alla Tua chiamata
Prima ero peccatore ma ora viaggerò
sulla strada del Signore
Signore sostienimi

 

 

Pokea Sadaka
(lingua: Swahili – Tanzania\Kenya)

Ee Bwana, pokea sadaka
tunayokutolea leo.
Mkate na divai Baba upo-okee
ni mazao yetu Baba upo-okee
Zigeuke mwili Baba upo-okee
na damu ya Yesu Baba upo-okee
Tupokee sisi Baba upo-okee
moyoni twatubu Baba upo-okee
Sadaka ya leo Baba upo-okee
ikupendeze tu Baba upo-okee
Ikusifu, Baba Baba upo-okee
ikukuze, Baba Baba upo-okee

Ricevi l’offerta e il sacrificio
che offriamo oggi
Pane e vino – ricevi Signore
sono i nostri frutti
Corpo e sangue di Gesù
Ricevici proprio dal cuore
Con l’offerta di oggi Ti sia dato amore
Ti diamo gloria, o Signore

 

 

Unastahili
(lingua: Swahili – Kenya)

Unastahili kuabudiwa unastahili Yesu,
unastahili kuabudiwa, unastahili eeh
Bwana wa mabwana
Bwana wa upendo
Mungu wa uwezo
Bwana wastahili

Ti dobbiamo ogni lode o Gesù,
Signore dei signori
Signore dell’amore
Dio della fortezza
Signore, a Te è dovuta

 

 

Wakati Wa Amani
(lingua: Swahili – Kenya)

Ni wakati wa amani, Yesu akupenda
amani yake Bwana, Yesu akupenda
wo wo wo wo wo wo – Yesu akupenda
ye ye ye ye ye ye – Yesu akupenda
Ni wakati wa shukrani…
Ni wakati wa shukrani…
Ni wakati wa faraja…
Ni wakati wa umoja…
Ni wakati wa upendo…
Ni wakati wa utendaji…
Ni wakati wa kilimo…
Ni wakati wa sadaka…

É il tempo della pace, Gesù ti ama
la pace del Signore, Gesù ti ama
É il tempo del grazie
É il tempo della consolazione
É il tempo dell’unione
É il tempo dell’amore
É il tempo del lavoro
É il tempo del raccolto
É il tempo dell’offerta